AJALI YA BASI YAUA WATANO, YAJERUHI 49 DODOMA

0
image
Ads

Watu watano wamepoteza maisha na wengine 49 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya AN Classic kugonga kwa nyuma lori la mizigo katika eneo la Chigongwe, jijini Dodoma.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Anania Amo, amesema ajali hiyo ilitokea jana saa nne usiku, ambapo basi lenye namba za usajili T405 BYS lililokuwa likiendeshwa na Swalehe Mnyapi lililigonga kwa nyuma lori la mizigo lenye namba T365 EDD, likiwa na tela T206 EEZ, wakati dereva wa basi alipokuwa akijaribu kulipita.

“Baada ya kugonga lori hilo, basi lilipoteza mwelekeo na kupinduka, hali iliyosababisha vifo vya watu watano na majeruhi 49. Kati ya hao, majeruhi 48 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, huku mmoja akihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa kwa matibabu zaidi,” amesema Kamanda Amo.

Ads

Ameongeza kuwa hali za majeruhi 11 ni mbaya zaidi, hasa kwa wale walioumia maeneo ya miguu. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo ili kubaini chanzo kamili na kuchukua hatua zinazostahili.

Spread the love
Ads

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *