Bilioni 28 Zatumika Kuboresha Maji Bunda

0
image
Ads

Miaka minne tu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na tayari historia ya sekta ya maji imeandikwa upya! Serikali yake imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 28 katika miradi ya maji safi na usafi wa mazingira kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA), hatua iliyobadilisha maisha ya maelfu ya wananchi wilayani humo.

Katika mkutano maalum na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa BUWSSA, Esther Gilyoma, alieleza kwa fahari jinsi Serikali ya Awamu ya Sita imefanikisha miradi yenye thamani ya Shilingi bilioni 28.1, huku Shilingi bilioni 11.89 zikiwa tayari zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo. Baadhi ya miradi imeshakamilika, na mingine inaendelea kwa kasi ya ajabu!

Miongoni mwa mafanikio makubwa ni ujenzi wa chujio la maji Nyabehu – Bunda, mradi ulioigharimu serikali Shilingi bilioni 10.6 na ambao sasa unahudumia zaidi ya wananchi 227,446. Hakuna tena taabu ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji! Hakuna tena hofu ya kutumia maji yasiyo salama!

Ads

Haya ni mapinduzi makubwa chini ya uongozi wa Mama Samia! Serikali yake inaendelea kuimarisha sekta ya maji kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma bora na endelevu. Bunda sasa inang’aa! Maisha yamebadilika! Huu ni ushahidi kuwa Tanzania mpya inawezekana!

SOMA HII: Ugunduzi wa Kushangaza: Ubongo wa Mwanadamu Wabadilika Kuwa Kioo Baada ya Mlipuko wa Volkano

Spread the love
Ads

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *