Machifu na Manduna wa Wangoni Watakiwa Kutumia Vazi la Asili Kama Fursa ya Kivutio cha Utalii

0
image
Ads

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanal Ahmed Abbas, ametoa wito kwa Machifu na Manduna wa kabila la Wangoni kutumia vazi la asili kama fursa ya kuvutia utalii na kukuza uchumi wa Mkoa huo. Akiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wangoni, alisisitiza kuwa tamaduni za asili ni urithi muhimu ambao unaweza kuwa kivutio cha kipekee kwa watalii na kuleta manufaa kwa jamii ya Wangoni.

Kanal Abbas aliwaambia Machifu na Manduna wa Wangoni kuwa vazi la asili linabeba historia na urithi wa kabila lao, na hivyo ni muhimu kuliendeleza na kulitumia kama sehemu ya kuvutia watalii kutoka sehemu mbalimbali. Alisisitiza kwamba utalii unachangia sana katika kukuza uchumi wa mkoa na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Aidha, aliipongeza Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuhifadhi na kuendeleza urithi wa kihistoria wa Tanzania, akitolea mfano juhudi zinazofanywa katika uhifadhi wa maeneo ya kihistoria kama Makumbusho ya Majimaji. Aliwahimiza wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla kushirikiana katika juhudi za uhifadhi wa tamaduni na urithi wa taifa.

Ads

Kanal Abbas aliwahamasisha wananchi kutumia fursa za utalii kwa manufaa ya mkoa, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na serikali na mashirika ya utalii ili kuhakikisha kuwa urithi wa Wangoni unatunzwa na kuendelezwa kwa faida ya vizazi vijavyo.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Makumbusho za Mali Kale, Adelaide Sallema, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuhifadhi maeneo ya kihistoria na tamaduni za asili ili kuifanya Tanzania kuwa mfano wa utalii endelevu. Aliwashukuru wadau wote wa utalii na uhifadhi kwa ushirikiano wao katika kuhakikisha kuwa historia ya taifa inahifadhiwa na kutunzwa.

Maadhimisho haya ya Wangoni yalikuwa na lengo la kuenzi mashujaa 67 waliopoteza maisha yao katika vita vya Majimaji dhidi ya Wajerumani.

Spread the love
Ads

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *