Wanawake wa WHI Watoa Msaada kwa Watoto Wenye Saratani TLM

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, wanawake kutoka Watumishi Housing Investments (WHI) walitembelea kituo cha @tlmtanzania kilichopo jijini Dar es Salaam, ambacho kinatoa huduma muhimu, ikiwemo msaada wa matibabu kwa watoto wanaosumbuliwa na saratani. Kituo hiki kimekuwa kikiwasaidia watoto wengi na familia zao kwa kuwapatia matibabu ya bure na huduma za ziada.
Wanawake kutoka WHI walikishukuru kituo cha TLM kwa huduma zao muhimu wanazozitoa kwa watoto na familia zao, huku wakionyesha mshikamano kwa kutoa michango mbalimbali. Walitoa msaada wa vitu mbalimbali, pamoja na fedha taslimu, ili kusaidia gharama za matibabu ya watoto waliopo katika kituo hicho.



Watumishi Housing Investment ni nini?
Watumishi Housing Investments (WHI) inatoa huduma ya kupangisha na kuuza nyumba kwa ajili ya makazi na biashara. WHI inauza aina mbalimbali za nyumba ambazo zinakidhi mahitaji ya mteja, zikianzia nyumba zenye vyumba viwili vya kulala hadi vyumba vinne. Nyumba hizo zinapatikana kwa aina mbalimbali, kuanzia zile za kujitegemea hadi zile zinazotegemeana.
Nyumba za WHI zimejengwa kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania na mahitaji ya maisha ya vijana. WHI ilifanya utafiti wa kutosha kabla ya kubuni michoro ya nyumba ilizojenga, hivyo muundo wa nyumba hizo umezingatia maoni na mapendekezo mbalimbali ya wateja. Kwa maombi maalum, mteja anaweza kuomba kufanyiwa marekebisho katika mchoro wa nyumba anayoitaka ili kuhakikisha inakidhi matakwa yake.
SOMA HII: Sababu Kuu Simba SC Kutoshiriki Mchezo Dhidi ya Yanga SC