Yanga SC Hawataki kupangiwa mechi siku ingine

Hali ya utata imeendelea kutawala kuhusu mchezo wa watani wa jadi, Yanga SC dhidi ya Simba SC, baada ya Yanga kusisitiza kuwa maandalizi ya mchezo huo yanaendelea kama ilivyopangwa, huku wakijivunia kuwa wenyeji wa mechi hii kubwa.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa Yanga SC, klabu hiyo imeeleza kuwa wanakubaliana na taratibu zote za mchezo kama zilivyoainishwa kwenye kanuni za Ligi Kuu ya NBC na kwamba maandalizi yote yamekamilika kwa ufanisi. Yanga, kama wenyeji wa mchezo, wamejizatiti kuhakikisha kuwa kila kitu kiko tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.
“Yanga SC itapeleka timu yake uwanjani kwa mujibu wa kanuni na taratibu za ligi, na tunasisitiza kuwa hatutakubali kucheza mchezo huu siku nyingine tofauti na leo,” imesema taarifa hiyo kutoka kwa uongozi wa Yanga SC.

Aidha, klabu hiyo imewataka wanachama, mashabiki, wapenzi wa klabu pamoja na wadau mbalimbali waliokuja kutoka mikoani, nchi za jirani na hata sehemu mbalimbali duniani kushiriki kwa wingi na kushuhudia mchezo huu wa kihistoria unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka.
Tunaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya mchezo huu huku tukiacha maswali yakiwa wazi:
- Je, hatua yoyote ya kisheria itachukuliwa baada ya matukio yaliyotokea?
- Je, mchezo huu utaathirika vipi na mashabiki waliojisajili tayari kutazama mechi hii?
SOMA HII: Sababu Kuu Simba SC Kutoshiriki Mchezo Dhidi ya Yanga SC