Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung, Afariki Dunia

0
image
Ads

Samsung Electronics imetangaza kifo cha Han Jong-Hee, Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, aliyefariki dunia Jumanne kutokana na mshtuko wa moyo. Han, mwenye umri wa miaka 63, alihudumu katika Samsung kwa zaidi ya miaka 37 na alikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kampuni, hasa katika biashara ya televisheni na vifaa vya kielektroniki.

Han aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics mwaka 2022, akisimamia biashara za vifaa vya kielektroniki na simu za mkononi. Kufuatia kifo chake, Jun Young-Hyun, ambaye aliteuliwa wiki iliyopita, atakuwa Mkurugenzi Mtendaji pekee wa Samsung.

Katika taarifa ya ndani iliyovuja kwa vyombo vya habari, Samsung ilimuenzi Han kama kiongozi aliyekuwa na mchango mkubwa katika kuifanya biashara ya televisheni za Samsung kuwa kinara wa dunia. “Tunatoa pole za dhati kwa familia yake na wapendwa wake katika kipindi hiki kigumu,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Ads

Samsung imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa katika sekta ya teknolojia, hasa kwenye biashara ya semiconductor. Wakati kampuni inatafuta kuimarisha nafasi yake sokoni, Han aliwahi kuomba radhi kwa wawekezaji kuhusu kushuka kwa hisa za Samsung na kueleza mipango ya kutafuta mikataba muhimu ya ununuzi wa kampuni (M&A) ili kusaidia ukuaji wake.

Han alijiunga na Samsung mwaka 1988 baada ya kuhitimu shahada ya uhandisi wa umeme kutoka Chuo Kikuu cha Inha. Kabla ya kuwa mkuu wa biashara ya vifaa vya kielektroniki, aliwahi kuongoza kitengo cha maonyesho ya skrini (display operation). Samsung ilimuelezea kama mtu aliyechangia ubunifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa televisheni za LED, ambazo zilisaidia kampuni hiyo kuendelea kuwa kiongozi wa teknolojia duniani.

SOMA HII: Siri yafichuka Waziri wa Watoto, Alizaa na Mtoto!

Spread the love
Ads

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *